Oct 4, 2022

MEYA KINONDONI AWATAKA WATANZANIA KUFANYA MAZOEZI TIBA

 


Meya Kinondoni  Awataka Watanzania  Kufanya Mazoezi tiba.

MEYA wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Songoro Mnonge ameiasa Jamii ya Kitanzania kuwa na desturi ya kufanya mazoezi  tiba angalau mara moja kwa wiki kwa manufaa yako mwenyewe.

Songoro aliyasema hayo alipoalikwa kuwa Mgeni rasmi wakati wa sherehe za maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Mazoezi tiba ya Kisiwani Clinic Centre(KCC) yenye makazi yake Mwananyamala Kinondoni jijini Dar es Salaam ambayo sherehe zake za kutimiza mwaka mmoja zilifanyika mwishoni mwa wiki Viwanja vya CCM ,Mwinjuma Mwananyamala Dar es Salaam.

Songoro aliipongeza KCC kwa juhudi inazozifanya za kusaidia jamii kwani wanaisadia Serikali kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wa magonjwa yasiyoambukizwa na Serikali imeliona hili.

Aidha Meya Songoro alimuomba Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni ambaye pia alihudhuria sherehe hizo kuwa mwakani watenge bajeti ya shughuli zinazofanywa na jamii kwa kujitolea kama hizi naye kama Meya atazisimamia kuhakikisha zinapitishwa kwa maufaa ya jamii badala ya vikundi kuchangishana.

Songoro alimaliza kwa kuwapongeza KCC kwa kazi kubwa waliyoifanya  ya kukusanya umati mkubwa wa kuhamasisha jamii kufanya mazoezi tiba na kuimba jamii basi ihamasike kweli kwani kauli mbiu ya maadhimisho haya kila mmoja inamhamasisha kweli afanye mazoezi kwani ni dhahili “Afya yako mtaji wako” ni kauli mbiu nzuri bila afya bora huwezi kuwa na manufaa kwa jambo lolote kwenye familia yako mpaka jamii inayokuzunguka.

Nae Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni alitoa shukrani kwa taasisi ya kujitolea ya KCC kwa kazi kubwa ya kukuzanya umati wa zaidi ya 2000 kuhamasisha jamii kufanya mazoezi kwa kauli mbiu ya “Afya yako Mtaji wako”

Pili aliahidi kushirikiana na KCC pamoja na vikundi vingine vya kusaidia jamii vyenye mlen go kama KCC Daima katika zoezi dhima la kuisaidia jamii kuondokana ama kupunguza magonjwa yasiyoambukiza.

Laiza alimaliza kwa kuahidi kushirikiana na Taasisi kwa kuwakilisha bajeti za vikundi kama KCC ili kupunguza maumivu ya vikundi kuchangishana ili kufanya hamasa ya kusaidia jamii ifanye mazoezi kwani tutakuwa tunaisaidia Serikali kufunguza Madawa ya kuhudumia Wagonjwa kadhaa wa magonjwa yasiyoambuza.

Nae mratibu wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mmoja wa KCC, Michael Machela  alishukuru kwa shughuli zote kufanyika kwa usalama na kwa kufana , ambapo maadhimisho yalihudhuliwa na vikundi vya Jogging 43 vyenye idadi ya Wanachama 25 mpaka 35 kila kikundi.

Lakini pia kulikuwa na Wananchi ambao walifuata huduma za matibabu mbalimbali zilizoalikwa katika maadhimishi hayo ambapo kulikuwa na JK Muhimbili ambao walikuwa wanatoa huduma za Magonjwa ya Moyo, Ocean Road wenyewe walikuja na huduma ya Saratani ya Mlango wa kizazi kwa kina Mama, Saratani ya Matiti kwa kina Mama na Saratani ya Tezi Dumea kwakina Wanaume, KAM wenyewe walikuja na huduma ya Kinywa na Manispa ya Kinondoni kupitia Hospitali ya Magomeni na Mwananyamala walikuja na huduma ya Macho, Sukari, Shinikizo la damu, kupima uzito, kuchangia damu pamoja na ushauri wa kitaalamu.

Kwa ujumla maadhimisho ya Kisiwani Clinic Centre yalihudhuliwa na Watanzania zaidi ya 2500 kutoka kona zote za jiji la Dar es Salaam.


Dec 18, 2015

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015

  


 Jumla ya wanafunzi 503,914 kati ya 518,034 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi,wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza,katika shule za sekondari za serikali katika awamu ya kwanza.Idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.3 ya wanafunzi waliofaulu na wenye sifa ya kujiunga na kidato cha kwanza



Dec 11, 2015

Video Mpya : Belle 9 – Burger Movie Selfie

http://www.hassbabytz.com/wp-content/uploads/2015/12/Belle-9-Burger-Movie-Selfie.png
                                                     

Nov 27, 2015

KAMISHNA MKUU WA TRA, RISHED BADE ASIMAMISHWA KAZI



  KAMISHNA MKUU WA TRA, RISHED BADE ASIMAMISHWA KAZI

Rais Dk Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania ( TRA) Rished Bade na kumteua Philiph Mpango kukaimu nafasi hiyo

Taarifa kutoka ikulu zimesema kuwa uamuzi huo wa Rais Magufuli umefuatia ziara ya waziri mkuu bandarini iliyobaini upotevu wa makontena 349.

Aidha Rais Magufuli amemtaka Rished Bade kutoa ushirikiano kwa Philiph Mpango wakati uchunguzi ukiendelea.

Mar 23, 2015

Mtoto awa mfungwa nyumbani kwao





                                                  Mtoto muathirika wa utesaji nyumbani 


Picha ya kushtusha imeachiliwa kwa ulimwengu hivi karibuni picha inayomuonesha mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitano aliye kondeana ,aliyetelekezwa katika sehemu ya chini ya nyumba yao ,aliyefungiwa na kuachwa afe njaa na familia yake.

Tammi Bleimeyer,mwenye umri wa miaka 33,na mumewe Bradley,mwenye miaka 24, wameshtakiwa kwa kosa la kuhatarisha uhai wa mtoto wao baada ya kumkuta mtoto huyo akiwa katika hali dhoofu katika majira ya baridi ,kitongoji cha Harris, huko Texas.

Askari aliye fanikisha kupatikana kwa mtoto huyo Mark Herman,amesema kwamba amefanya kazi ya polisi katika kipindi cha miaka thelathini lakini hajawahi kushuhudia tukio lanamna hii.

Askari huyo anasema wamemkuta mtoto huyo katika hali mbaya ana njaa kali,amekondeana,amevilia damu mwilini kama aliyekuwa akipigwa ama kupitia mateso makali na ngozi yake ilionekana kama imeachana na mifupa ,ilikuwa ni hali ya kutisha sana kumwona mtoto katika hali hiyo.

Bradley alikuwa akibishana na mtoto huyo wa kambo mwenye umri wa miaka kumi na sita aliyekuwa akiwataka wazazi wa mtoto huyo kuacha kumfungia mtoto wako katika chumba cha chini ya ardhini nyumbani mwao .

Na polisi walipofika nyumbani hapo waligundua chumba kidogoo,chini ya nyumba hiyo kikiwa kimefungwa na godoro tu ndani yake na mtoto aliyeketi juu ya godoro ,ingawa mama wa kambo wa mtoto huyo alimtorosha baada ya kujua kwamba polisi wanamfuatilia, na kumkuta katika chumba cha hoteli na kumfuatilia hatimaye kumchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitalini kwa matibabu.

Ingawa mpaka mtoto huyo anafikishwa hospitalini, sababu za kufungiwa kwa mtoto huyo hazikufahamika mara moja ,na wazazi wa mtoto huyo wamekataa kuzungumzia tukio hilo .

Baba wa mtoto huyo anashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo, na mtoto wake bado amesalia hospitalini kwa matibabu zaidi katika hospitali ya watoto iliyoko mjini Texas .

chanzo na  http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

HUYU NDIO MWENYEKITI MPYA WA PAC KAMATI ALIYOKUWA ANAIONGOZA ZITTO KABWE




Kamati ya Bunge ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma (PAC), imemchagua Mhe. Amina Mwidau (MB) kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati hiyo kuchukua nafasi ya Mhe. Zitto Kabwe ambaye si mbunge tena.

Mhe. Mwidau ni Mbunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Wananchi CUF kutoka mkoa wa Tanga, ni msomi mwenye stashahada ya Diplomasia ya Biashara, Shahada ya Biashara na Shahada ya Uzamili ya Biashara.

TUNAMTAKIA KILA LA KHERI KATIKA NAFASI YAKE HII

Dec 1, 2014

VIDEO MPYA YA Lady jaydee ft Dabo Forever (Official Video HD/2k/4k)




EMERSON ASAINI YANGA RASMI LEO

Kiungo mbrazil Emerson De Oliviera Neves Roque (kushoto) akisaini mkataba leo wa kuitumikia klabu ya Young Africans, kulia ni Afisa Habari wa klabu Baraka Kizuguto   

Kiungo Emerson De Oliveira Neves Roque leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Young Africans baada ya benchi la ufundi kuridhika na uwezo wake,na mchezaji mwenyewe kufikia makubaliano hayo ya kuwatumikia watoto wa Jangwani.

Baada ya kufanya mazoezi kwa siku nne mfululizo chini ya makocha Marcio Maximo, Leonardo Neiva na makocha wazawa Salavatory Edward, Shadrack Nsajigwa kwa pamoja wameridhiswa na uwezo wake na kuomba apewe kandarasi la kuitumikia klabu ya Young Africans.

Emerson aliyekua akichezea katika timu ya Bonsucesso iliyopo daraja la pili kwenye jimbo la Rio de Janeiro anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santos "Jaja" ambaye ameshindwa kureje nchini kutokana na matatizo ya kifamilia na kuomba klabu ya Young Africans imuache.

Kocha wa Young Africans Marcio Maximo amesema wamerizishwa na uwezo na kiungo mkabaji Emerson na kusema ataisaidia timu katika michuano mbali mbali ya Ligi na Kimataifa. 

Ujio wa Emerson unafanya klabu ya Young Africans kufikisha jumla ya wachezaji watano wa kimataifa, wengine wakiwa ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kizza na Andrey Coutinho.

Oct 22, 2014

Vyanzo: Sakata la Diamond kuvaa sare za jeshi, Babu Tale ashikiliwa na polisi, Kamanda wa polisi azungumza

Vyanzo: Sakata la Diamond kuvaa sare za jeshi, Babu Tale ashikiliwa na polisi, Kamanda wa polisi azungumza

Kufuatia tukio la Diamond Platinumz kuonekana akiperform na sare zinazoaminika kuwa za jeshi la Wananchi (JWTZ), imeelezwa kuwa jeshi la Polisi limemshikilia meneja wa Diamond, Babu Tale na inaelezwa kuwa alilala selo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwa katika eneo la kituo cha polisi cha Osterbay, Dar es Salaam jana (October 21), Babu Tale alifikishwa katika kituo hicho ambapo maafisa kadhaa wa jeshi na polisi walionekana katika eneo hilo.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa Uongozi wa Diamond ulipewa muda wa kujieleza kabla ya saa mbili asubuhi, October 21 lakini haukufanya hivyo na ndipo hatua hiyo ikachukuliwa.

Haijafahamika bado kwa nini jeshi la Polisi lilimshikilia Babu Tale peke yake bila Diamond lakini vyanzo vimeeleza kuwa mwanamuziki huyo yuko safarini.

Hadi habari hii inaenda hewani, namba ya simu ya Babu Tale ilikuwa haipatikani.

Tovuti ya Times Fm imeongea na kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Dar es Salaam, Camillus Wambura ambaye amesema bado hajawasiliana na kituo cha Osterbay kuhusu suala hilo na hajapata taarifa kwa kuwa kesi hiyo inachunguzwa na iko chini ya mkuu wa upelelezi wa Mkoa.

“Mimi ninachojua kuwa suala hilo liko chini ya uchunguzi. Habari ya kushikiliwa watu na nini bado sijafahamu. Najua tu  suala hilo liko chini ya uchunguzi na linafanyiwa uchunguzi. Hiyo ni kesi ambayo iko chini ya mkuu wa upelelezi wa Wilaya, chini ya mkuu wa upelelezi wa Mkoa. Kwa hiyo sijapokea taarifa ya uchunguzi huo ulipofika.” Ameiambia tovuti ya Times Fm.

Akijibu kuhusu taarifa za uongozi wa Diamond na Diamond kupewa muda wa kujieleza, Kamanda Wambura alijibu:

“Uchunguzi unafanywa huko. Kwa sasa hivi sina taarifa hiyo nina mambo mengi sana. Kwa hiyo kwa sasa hivi uchunguzi unafanywa chini ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa. Kwa hiyo sijapata nafasi ya kujua wamefikia wapi katika uchunguzi wa suala hilo,”ameongeza kamanda Wambura.

Mapema wiki hii, jeshi la wananchi Tanzania lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari likipiga marufuku raia kuvaa sare za jeshi.

chanzo na http://timesfm.co.tz

Oct 21, 2014

Mwanariadha Oscar Pistorius ahukumiwa kwenda jera miaka 5







Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.

Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya mauaji bila ya kukusudia.

Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.

Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.

Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.

Upande wa mashitaka ulisisitiza Pistorius afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.

Jaji alisema kuwa Pistorius asingepewa adhabu ya kifungo cha nyumbani kwani hukumu kama hiyo ingekuwa hatua mbaya na mfano mbaya kwa wahalifu.